Imetoka kwa Ibn Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mjumbe wa Allaah amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy].
Bimaana akafa Shahiid kwenye Vita vya Jihad,huyo ndie mwenye fadhili kuliko masiku haya Mtume Swalla llahu aleyhi waslam aliyapimia hivyo.
Zifuatazo ni fadhila kuu za masiku hayo kumi ya Dhul-Hijjah. Na lau ee ndugu Muislamu utakapojipwekesha katika ibaada na kutenda amali njema zenye ikhlaas na zinazotokana na mafunzo Sahihi ya Sunnah za Mtume (Swalla-Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi bila shaka utajichumia thawabu maradufu na ambazo zitakuwa nzito In Shaa Allaah katika mizani yako.
Kwa jinsi zilivyokuwa na umuhimu mkubwa siku hizo kumi, hadi kwamba Allaah (Subhaanah wa Ta'ala) Ameziapia katika Qur-aan Anaposema:
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ((وَالْفَجْرِ)) ((وَلَيَالٍ عَشْرٍ))
BisimiLLaahir-Rahmaanir-
Wanavyuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo ni Siku kumi za Dhul-Hijjah.
Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’ala) kwa kukumbuka Neema Zake zisizohesabika:
((لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ))
((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28].
Ibn ‘Abbaas kasema: "Hizo ni siku kumi za Dhul-Hijjah” . Na Amesema: "Manufaa ya dunia hii na ya Akhera” . Manufaa ya Akhera yanajumuisha kupata Radhi za Allaah. Manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].
Fadhila yaliyomo ndani ya masiku 10 ya mwezi wa Dhul-Hijjah na Mafundisho yake.
Assalamu aleykum warahmatullahi wabarakatu,fadhila za masiku kumi ya mwezi wa Dhul Hijjah yameanza September 25,2014.