Afisa wa Polisi auawa katika mji wa Mombasa na watu 5 watekwa Lamu.

Saturday October 11, 2014 - 21:38:58 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2402
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 1 0
  • Share via Social Media

    Afisa wa Polisi auawa katika mji wa Mombasa na watu 5 watekwa Lamu.

    Kumepatikana maelezo zaidi kuhusiana na shambulio lililofanyika masaa machache yaliopita nchini Kenya ambapo miaka ya hivi karibuni ulishuhudia hali mbaya ya kiusalama.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kumepatikana maelezo zaidi kuhusiana na shambulio lililofanyika masaa machache yaliopita nchini Kenya ambapo miaka ya hivi karibuni ulishuhudia hali mbaya ya kiusalama.Habari kutoka mji wa Pwani wa Mombasa zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha walimwua Afisa wa Polisi kwenye Hoteli mmoja inayojulikana Royal Court katikati mwa mji wa huo.
Mauaji hayo yanakuja wakati kukiwa na hali ya tahadhari mkubwa kwa mashirika yote ya Usalama nchini Kenya,mamia ya Maaskari wa usalama wamepelekwa kwenye baadhi ya mitaa na maeneo muhimu ili kuepuka na mauaji ya kupangwa na Milipuko ya mara kwa mara lakini hatua hiyo inaonekana kufeli baada ya Afisa mwenye cheo kuawa mjini Mombasa leo.Naibu Kamishna wa Polisi katika Mkoa wa Pwani amewaambia vyombo vya habari kuwa wataanza uchunguzi namna alivyouawa afisa wake wa Polisi aliyeuawa katikati mwa mji wa Mombasa.Upande mwingine watu waliojihami na silaha wamefanya shambulio na kuteka watu nje kidogo na Kisiwa cha Lamu,Duru za kuaminika zinaeleza kuwa watu 5 wametekwa kwenye Kijiji kilicho karibu na Kisiwa hicho cha Lamu.Habari zaidi zinaeleza kuwa watu waliotekwa wamechukuliwa kutoka kwenye Gari mmoja iliyokuwa imebeba Miraa ambapo ilitokea upande wa mji wa Nairobi,Maofisa wa Polisi nchini Kenya wameilamu Al-Shabab kwa kutekeleza mashambulio hayo.Si mara ya kwanza kufanyika shambulio katika Kiswa hicho cha Kitalii nchini Kenya,mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Harakat Al-Shabab Al Mujahideen kuhusiana na mashambulio hayo mapya.Related Items