Maelezo:Maaskari na Maofisa wa Serikali ya FG wauawa katikati mwa Mji wa Mugadishu.

Monday November 03, 2014 - 23:09:01 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2009
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 1 0
  • Share via Social Media

    Maelezo:Maaskari na Maofisa wa Serikali ya FG wauawa katikati mwa Mji wa Mugadishu.

    Mauaji ya kupangwa yametokea masaa machache yaliopita katika baadhi ya mitaa ya mjini Mugadishu ambao ni ngome ya Wanajeshi wa AMISOM na Wanamgambo wa Serikali ya Hassan Sheikh.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Mauaji ya kupangwa yametokea masaa machache yaliopita katika baadhi ya mitaa ya mjini Mugadishu ambao ni ngome ya Wanajeshi wa AMISOM na Wanamgambo wa Serikali ya Hassan Sheikh.Vikosi vya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen walifanya shambulio dhidi ya Gari walilokuwemo Maaskari wa Serikali kwenye eneo la Makutano ya Zope Wilayani Wadajir na shambulio hilo waliuawa Maaskari 3 na wengine 4 wakijeruhiwa vibaya.
Mauaji yaliofanyika Barabara kuu ya Lami ya Taleeh Wilayani Hodon ameuawa Afisa mmoja wa Serikali ya Hassan Sheikh baada ya kushambuliwa Gari alilokuwemo na mtu mmoja aliyokuwemo kwenye Gari hilo amejeruhiwa lakini mpaka sasa hakuna maelezo zaidi kuhusiana na mauaji hayo.Shambulio lingine iliyofanyika Wilaya ya Wadajir ameuawa Kiongozi mmoja wa Wizara ya mambo ya nje wa Serikali ya FG na alikuwa akiitwa Mohamed Abdi Jogos.Upande mwingine kuna taarifa zinazogongana kuhusiana na mauaji ya Wasichana wawili waliokuwepo katika Wilaya ya Darkinley mjini Mugadishu.Duru ziliarifu kuwa watu waliokuwa na silaha walifanya mauaji hayo na baada ya muda mfupi waliondoka eneo hilo,Wasichana hao waliouawa inasemekana walikuwa wakifanya kazi mmoja ya Wizara za Serikali ya FG lakini vyombo vya habari vinayozungumza kwa niaba ya Serikali ya Hassan Sheikh vilitangaza kuwa Wasichana waliouawa walikuwa ni Wanafunzi waliokuwa wakisoma mmoja ya Shule za mjini Mugadishu.Baadhi ya Barabara mjini Mugadishu umefungwa na walionekana Maaskari wa Kisomali na Wanajeshi wa AMISOM wakizuia Magari yanayotumiwa na Wananchi.


Barabara ya lami unaopita eneo la Majengo ya Uturuki Wilayani Hodon umefungwa kwa mawe na Wananchi walionekana wakitembea kwa miguu katika barabara walizozibuni.

Related Items