Marekani yawaonya Raia wake kusafiri kwenda nchini Kenya.

Saturday June 21, 2014 - 08:16:31 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 1949
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 1 0
  • Share via Social Media

    Marekani yawaonya Raia wake kusafiri kwenda nchini Kenya.

    Taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema na kuwaonya Raia wake wanaotaka kusafiri kwenda nchini Kenya iliyo kwenye Bara la Afrika Mashariki.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema na kuwaonya Raia wake wanaotaka kusafiri kwenda nchini Kenya iliyo kwenye Bara la Afrika Mashariki.
Marekani imesema wamepata taarifa ya kijasusi inayolenga kushambulia maslahi ya Marekani na hivyo hakuna budi kuzuia wanancho wote wa nchi hiyo kuzuiwa Safari zao kwenda nchini Kenya.

"Mabadiliko upande wa Usalama uliopo nchini Kenya imetulazimu kuwahamisha wafanyakazi wa Ubalozi wetu huko Raia wetu tukiwaonya kusafiri kwenda katika nchi hiyo",ilisema sehemu ya taarifa iliyotolewa na Wizara ya Masuala ya Nje wa Marekani.


Mashirika ya Usalama wa Marekani wameonya uwezekano wa kutokea Mashambulio kama ule wa wiki uliopita kwenye mji wa Mpeketoni Kisiwani Lamu iliyowaua watu zaidi 70 na Al-Shabab ilikiri kuhusika na Shambulio hilo.

Kwenye miji iliyowaonya Marekani dhidi ya Raia wake kwenda kusafiri ni pamoja na Mji wa Pwani wa Mombasa,Kwale,Kilifi,Lamu na Katika Mkoa wa Tana River nchini Kenya.


Upande mwingine Waziri wa Masuala ya ndani wa Kenya amewatahadharisha Wananchi wa Kenya kutokwenda kwenye mikusanyiko wa sehemu za kuangalia Mechi ya Kandanda unaoendelea nchini Barazil onyo hii ya Kenya imeitaja kuwa ni tahadhari upande wa Kiusalama kutokana na Uwezekano wa kutokea mashambulio makubwa katika siku za usoni.

Related Items