Wanajeshi wa Ethiopia wafurushwa mji wa Wabho na Mujahidina wa Al-Shabab wadhibiti mji huo.

Tuesday December 16, 2014 - 09:57:17 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2802
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 1 1
  • Share via Social Media

    Wanajeshi wa Ethiopia wafurushwa mji wa Wabho na Mujahidina wa Al-Shabab wadhibiti mji huo.

    Habari kutoka mkoa wa Galgaduud katikati mwa Ardhi ya Somalia zinaeleza kuwa mapiagno yalioanza tokea jana yamekamilika kwenye mji wa Wabho.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Habari kutoka mkoa wa Galgaduud katikati mwa Ardhi ya Somalia zinaeleza kuwa mapiagno yalioanza tokea jana yamekamilika kwenye mji wa Wabho.Mapigano hayo yalikuja wakati Wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa Wabho kujaribu kuelekea mji wa Mahaas na kisha Mujahidina wa Al-shabab kuwavizia njiani.
Habari za mwishone zinaeleza kuwa mji wa Wabho tayari umedhibitiwa na Mujahidina huko Wanajeshi wa Ethiopia wakielekea upande wa mji wa Mahaas wakiwa wamevunjwa migongo.Taarifa rasmi uliotolewa na Wilayatul Islamiah ya Galgaduud imeleza kuwa tayari mji wa Wabho uko chini ya utawala wa Kiislaam huko vikosi vya Mujahidina wakipongezwa hatua hiyo ya kuwafurusha Maadui.Sheikh Hassan Ya'qub ambae ni mwakilishi wa Kiislaam katika mkoa wa Galgaduud amezungumza na Idhaa ya Kiislaam ya Radio Al Andalus na amethibitisha kuwa Wanajeshi wa Ethiopia wamefurushwa kutoka mji wa Wabho huko akitoa sababu ya kufurushwa kwao ni kuwekewa vizuizi vya muda mrefu na mashambulio ya mara kwa mara,"Tunamshukuru Allah kwa kuwaondoa Wanajeshi wa Ethiopia katika mji wa wabho,ikiwa watarudi basi watakutana na yale kile walichokionja hapo awali,na kama wataacha kuja basi ni shukrani kwa Allah ta'alaa",alimalizia Sheikh Hassan Ya'qub.
Related Items