Wanajeshi wa Siaralione watarajiwa kuondoka kwenye mkoa wa Jubba na taarifa zisemayo kuwa Wanajeshi wa Ethiopia kuchukua mji wa Kismaayo.

Friday December 19, 2014 - 21:49:22 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2186
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 0 1
  • Share via Social Media

    Wanajeshi wa Siaralione watarajiwa kuondoka kwenye mkoa wa Jubba na taarifa zisemayo kuwa Wanajeshi wa Ethiopia kuchukua mji wa Kismaayo.

    Habari kutoka mji wa Kismaayo makao makuu ya mkoa wa Jubba kusini mwa Ardhi ya somalia zinaeleza kuwa Wanamgambo wa Ahmed Madobe na Wanajeshi wavamizi kutoka nchini Kenya wametangaza hali ya kutotoka nje kwenye baadhi ya mitaa ya mji huo.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Habari kutoka mji wa Kismaayo makao makuu ya mkoa wa Jubba kusini mwa Ardhi ya somalia zinaeleza kuwa Wanamgambo wa Ahmed Madobe na Wanajeshi wavamizi kutoka nchini Kenya wametangaza hali ya kutotoka nje kwenye baadhi ya mitaa ya mji huo.Maeneo ya soko pamoja na biashara mjini Kismaayo yalifungwa huko barabara zilizokuwa na changamkeni zikifungwa wanajeshi wa Kenya na yale ya Ahmed Madobe walionekana wakiwazuia wananchi kutumia Barabara hizo.
Ujumbe uliokuwa ukiongozwa na Hassan Sheikh kiongozi wa Serikali ya FG ulitua katika uwanja wa Ndege wa mji wa Kismaayo,Duru zilieleza kuwa Hassan Sheikh alishiriki hafla ya kuwasindikiza Wanajeshi wa Siaralione ambao siku za hivi karibuni wanatarajiwa kuondoka baadhi ya miji ya Mkoa wa Lower Jubba kusini mwa Somalia.Habari zaidi zinaeleza kuwa Maofisa wakuu wa kijeshi wa Serikali ya Ethiopia wako kwenye mji wa Kismaayo huko kukiwa na mpango wa kupelekwa Wanajeshi wa Ethiopia katika mji wa Kismaayo.Taarifa zinadai kuwa Wanajeshi wa Kenya wataondolewa kutoka mji wa Kismaayo na wanatarajiwa kupelewa kwenye miji ya Tabto,Afmadow,hadi katika mji wa Dobley ambapo Wanajeshi wa Siaralione wanatarajiwa kuacha wazi.Kulikuwa na hali ya kutoelewana baina ya mataifa ambao Wanajeshi wao wameivamia Ardhi ya Somalia ndani ya miezi ya hivi karibuni ambapo inahusiana na mshahara wanaopata kutoka kwa U.N.

Related Items