Obama Alia na Dola ya Kiislaam na Al Qaida asema hawawakilishi Uislaam!

Friday February 20, 2015 - 09:13:49 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 3738
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 45
  • 1 0
  • Share via Social Media

    Obama Alia na Dola ya Kiislaam na Al Qaida asema hawawakilishi Uislaam!

    Kiongozi wa serikali ya Marekani Barack Obama ameonyesha wasiwasi wake kuhusiana na ukuaji mkubwa wa Mujahidina kote duniani na athari zinazoweza kupatika katika mataifa ya Kiislaam.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kiongozi wa serikali ya Marekani Barack Obama ameonyesha wasiwasi wake kuhusiana na ukuaji mkubwa wa Mujahidina kote duniani na athari zinazoweza kupatika katika mataifa ya Kiislaam.Alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kimataifa uliokuwa ukizungumzia kwa kile walichokiita Misamamo mikali na Ugaidi amesema Mujahidina wa Dola ya Kiislaam na Al-Qaida wamekuwa uwezo pekee unaowalinda waislaam.
Obama ameonyesha na kuwaelezea washiriki wa mkutano huo kuwa wasiwasi wake alionayo juu ya Mujahidina kwa kuwavutia na kuwaunga mkono waislaam Bilioni mmoja kote Duniani."Dola ya Kiislaam na Al-Qaida wanatafuta uungwaji mkono wa waislaam huko wakijifanya kuwalinda lakini ilhali hawako hivyo ni watu wenye misimamo mikali na wala wahawakilishi Uislaam",alisema Obama.Barack Obama alikuwa akizungumza kama vile mashekhe waovu wanavyozungumza lakini amekiri wapiganaji wa Kiislaam ndio watu pekee waliowavuta waislaam kote duniani."Watu hao wenye misimamo mikali hawana uwakilishi wowote kwa waislaam kwasababu Uislaam ni Amani",aliendelea kusema Obama.Alipogusia vita vya Marekani dhidi ya waislaam amekiri jambo hilo lakini ameigeuza na kufanya vita hivyo ni dhidi ya waislaam wenye misimamo mikali "Marekani hayuko vita dhidi ya waislaam bali vita vyake ni dhidi ya walio na misimamo mikali waliopinda na vita hivyo ni sisi na waislaam kwa pamoja tukipigana dhidi ya hao walio na misimamo mikali ya kidini",alimazlizia Obama.Taarifa hii ya kiongozi wa Marekani inakuja wakati ambapo Dola ya Kiislaam imeweza kupata umaarufu katika mataifa ya kiislaam Duniani na pia makundi ya kijihadi yalio na mahusiano na Al-Qaida kujipanua zaidi kote Duniani.

Related Items