Yemen yaomba msaada wa Kijeshi kutoka nje na Saudia yawaonya wanamgambo wa Kishia wa Huthi.

Tuesday March 24, 2015 - 22:23:50 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2718
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 40
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Yemen yaomba msaada wa Kijeshi kutoka nje na Saudia yawaonya wanamgambo wa Kishia wa Huthi.

    Baada ya wanamgambo wa Kishia wa Huthi walio mawakala wa Iran kuutwaa miji mikubwa pamoaja na mji mkuu wa San'aa nchini Yemen Serikali kibaraka ya nchi hiyo sasa imeomba msaada wa kijeshi kuingilia masuala ya ndani ya Yemen.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Baada ya wanamgambo wa Kishia wa Huthi walio mawakala wa Iran kuutwaa miji mikubwa pamoaja na mji mkuu wa San'aa nchini Yemen Serikali kibaraka ya nchi hiyo sasa imeomba msaada wa kijeshi kuingilia masuala ya ndani ya Yemen.Naibu waziri wa masuala ya kimataifa nchini Yemen Riyadh Yasin ametangaza rasmi kuwa wanawaomba mataifa ya muungano wa nchi za kiarabu ya Khaleaj uingiliaji wa haraka wa Kijeshi nchini humo.
Utawala wa Yemen imesema Uhuru wa uwepo kwa Serikali ya nchi hiyo iko hatarini baada ya wafuasi wa Iran kuanza uvamizi mpya katika mikoa ya Kusini mwa nchi hiyo ya Yemen ambao ilikuwa maeneo yaliosalimika kwa wanamgmbo hao wa kishia wa Huthi."Yemen inawaomba Serikali za muungano wa nchi za Kiarabu Khaleaj kuchukua hatua za haraka ikiwa itafeli mazungumzo yanayoendelea hivi sasa wanamgambo wa Huthi ni lazima waondolewe kutoka na uwepo uhuru wa nchi ya Yemen",alisema Riyadh Yasin.Upande mwingine waziri wa Masuala ya kimataifa wa Utawala wa Aala Saudi Saudi Al Feysal ametangaza mjini Riyadh kuwa Serikali yake itawachukulia hatua kali endapo wanamgambo wa Huthi wataendelea na kile alichokiita Uvunjifu wa usalama katika Mkoa.Utawala wa Aala Saudi na Muungano wa nchi za kiarabu inasemekana wako kwenye juhudi ya kuwaingiza Wanajeshi wa Mataifa ya nchi za Khaleaj unaojulikana Dar'ul Jazeerah" kuingilia kijeshi nchini Yemen na kujaribu kuwafurusha wanamgambo wa Kishia wa Huthi kutoka katika mikoa ya Adan na Lahaj.Hatua hii inakuja wakati ambapo wafuasi wa Jamhuri ya Kishia wa Iran kuiteka mji wa 3 kwa ukubwa nchini Yemen na kuanza uvamizi mpya dhidi ya Rabih Hadi Mansuur kiongozi wa nchi hiyo aliye uhamishoni.Ijumaa iliyopita milipuko mikubwa yaliofanyika katika misikiti miwili yameua watu zaidi ya 147 ambapo wote walikuwa wanamgambo wa Kishia wa Huthi pamoja na wafuasi wao.

Related Items