Serikali ya FG yahofia Al-Shabab kuteka maeneo walioachia AMISOM.

Friday March 27, 2015 - 09:23:57 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2152
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 40
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Serikali ya FG yahofia Al-Shabab kuteka maeneo walioachia AMISOM.

    Katika siku tatu zilizopita Wanajeshi wa Kigeni waliojiita AMISOM walikuwa wakijiondoa baadhi ya Miji na Vijiji viliopo mkoani Lower Shabelle.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Katika siku tatu zilizopita Wanajeshi wa Kigeni waliojiita AMISOM walikuwa wakijiondoa baadhi ya Miji na Vijiji viliopo mkoani Lower Shabelle.Makaazi ya mwisho walioachia wanajeshi hao wavamizi ilikuwa Sabib iliyo karibu na mji wa Afgooye,wanamgambo wa Serikali ya FG wameachiwa katika miji ya Awdeegle na Barire.
Abdilqadir Sidii ambae ni mwakilishi wa Mkoa wa Lower Shabelle upande wa Serikali ya FG ameonyesha khofu yake katika baadhi ya maeneo Muhimu walioachia AMISOM kudhibitiwa na Al-Shabab.Sidii ambae alizungumza na Idhaa ya VOA amethibitisha kuwa wanajeshi wa AMISOM wameachia maeneo mengine mapya huko hatua hiyo akitaja kuwa ni hatua iliyoharakishwa."Wanajeshi wa AMISOM bila kujulikana ghafla wameondoka kutoka miji ya Awdigle,Barire pamoja na Sabiib,na hawajatupa taarifa yeyote,na tulipojaribu kuwauluza hatua yao hiyo wametujibu kuwa kulikuwa na makubaliano ya 22 June kati yao na Serikali ya Somalia ambao ilikuwa inataja kuwa maeneo yote wanaoachia wawe tayari wamekwisha kabidhiwa Wanajeshi wa Serikali",alisema Abdilqadir Sidii.Maofisa wa Serikali ya FG inayofanya kazi na wavamizi wa kigeni wanakhofia maeneo yote walioachia wanajeshi wa AMISOM kudhibitiwa na Al-Shabab.

Related Items