Ndege ya kivita ya Saudi Arabia yaanguka katika Bahari ya Aden na Marekani yatoa msaada kwa Marubani.

Saturday March 28, 2015 - 21:19:18 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 3127
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 5
  • 0 1
  • Share via Social Media

    Ndege ya kivita ya Saudi Arabia yaanguka katika Bahari ya Aden na Marekani yatoa msaada kwa Marubani.

    Wizara ya ulinzi wa Utawala wa Saudi Arabia imetangaza kuwa ndege yake ya kivita iliyokuwa ikishirika vita dhidi ya wanamgambo wa Kishia wa Huthi nchini Yemen imeanguka ktika Bahari ya Aden.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Wizara ya ulinzi wa Utawala wa Saudi Arabia imetangaza kuwa ndege yake ya kivita iliyokuwa ikishirika vita dhidi ya wanamgambo wa Kishia wa Huthi nchini Yemen imeanguka ktika Bahari ya Aden.Ndege hiyo aina ya F15S ilianguka ghafla na baadae Marubani wawili wa ndege hiyo walitumia kiangushio/parachute na kuangukia Baharini.Waziri wa Ulinzi wa Utawala wa Saudi Arabia Mohamed Bin Salmaan amewaambia vyombo vya habari kuwa Marubani hao waliokolewa na wanajeshi wa Marekani Barani Afrika katika kituo cha nchi ya Djibuti.


Marubani hao waliokuwa wakiongoza ndege wote wamejeruhiwa,Utawala wa Riyadh unaongoza ushirika unaowajumuisha mataifa 10 ya nchi za kiarabu na kuivamia Yemen ikiwa ni hatua mmojawapo ya kuwaondoa wanamgambo wa Kishia wa Huthi ambao wamekuwa tishio kwa Serikali dhaifu ya Yemen.


Ndege hiyo ya utawala wa Saudia Arabia ina bei ya juu na inasemekana katika masoko ya ndege ya kivita ndege hiyo ya F15S ina thamani ya Dola za kimarekani milioni 27.

Related Items