Serikali ya Ethiopia yatangaza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka jimbo la Hiraan Somalia.

Tuesday March 31, 2015 - 09:42:31 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 1800
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 30
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Serikali ya Ethiopia yatangaza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka jimbo la Hiraan Somalia.

    Uongozi wa kijeshi wa Ethiopia waliopo jimbo la Hiraan katikati mwa Ardhi ya Somalia wametangaza kuondoka kutoka vijiji na miji yote ya Jimbo hiyo ya Hiraan.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Uongozi wa kijeshi wa Ethiopia waliopo jimbo la Hiraan katikati mwa Ardhi ya Somalia wametangaza kuondoka kutoka vijiji na miji yote ya Jimbo hiyo ya Hiraan.Hafla fupi iliyofanyika nje kidogo na mji wa Beledweyne maofisa wa kijeshi wa Ethiopia wametangaza rasmi kuwa wanaondoka mkoa wa Hiraan baada ya kuishikilia kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu kwa kutumia jina la AMISOM ambapo walishikilia kwa nguvu miji ya Mahaas na Beled Weyne.Naibu kamanda wa Jeshi la AMISOM ambae ni Mganda kwa upande wake amethibitisha kuondoka kwa Wanajeshi wa Ethiopia kutoka Jimbo la Hiraan,Abdil fatah Afrah ambae Ethiopia ilimpa kiti cha kuwa Mkuu wa mkoa wa Hiraan nae kwa upande wake amewathibitishia vyombo vya habari na kusema kuwa Wanajeshi wa Ethiopia walimpa taarifa ya kuondoka Hiraan na ameonyesha wasiwasi wake kuhusiana na hatua ya Ethiopia ya kuondoka kutoka mkoa wa Hiraan katikati mwa Ardhi ya Somalia.


Siku chache zilizopita vikosi vya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen waliutwaa eneo la Buq Gosaar iiyo nje kidogo na mji wa Beledweyne baada ya wanajeshi wa Ethiopia waliokuwepo eneo hilo kuondoka.

Related Items