Mwendesha mashtaka wa Kesi za Ugaidi nchini Uganda auawa mjini Kampala.

Wednesday April 01, 2015 - 23:20:04 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2335
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 35
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Mwendesha mashtaka wa Kesi za Ugaidi nchini Uganda auawa mjini Kampala.

    Watu waliokuwa na silaha wamempiga risasi na kumwua katikati mwa jiji la Kampala mwendesha mashtaka wa kesi za ugaidi katika Mahakama kuu nchini Uganda.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Watu waliokuwa na silaha wamempiga risasi na kumwua katikati mwa jiji la Kampala mwendesha mashtaka wa kesi za ugaidi katika Mahakama kuu nchini Uganda.Habari kutoka nchini Uganda zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha ambapo walikuwa na Boda Boda wamempiga risasi hadi kufa mwana mama Joan Kagezi aliyekuwa ndani ya Gari lake Ndogo mjini kampala.
Mashuhuda walionukuliwa na vyombo vya habari nchini Uganda zinaeleza kuwa mwanamama huyo alipigwa risasi ya kichwani na baadae alikufa kabla hajafikishwa Hospitali kuu ya mjini Kampala.Joan Kagezi alikuwa akijiandaa kuwafungulia mashtaka waislaam wapatao 13 ambapo wanatuhumiwa kuwa na mahusiano na kundi la Harakat Al-Shabab Al Mujahideen na kuhusishwa mashambulio yaliosababisha hasara ya mwaka 2010.Mkuu wa Polisi nchini Uganda amesema wamesikitishwa na kifo cha Joan Kagezi na kumtaja kuwa shujaa aliyekuwa na umuhimu mkubwa katika usalama wa nchi ya Uganda.

Related Items