Raila Odinga "Wanajeshi wa Kenya ni lazima waondolewa haraka kutoka Somalia ili kuepuka Mashambulio ya Al-Shabab".

Tuesday April 07, 2015 - 22:03:55 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 3776
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 42
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Raila Odinga "Wanajeshi wa Kenya ni lazima waondolewa haraka kutoka Somalia ili kuepuka Mashambulio ya Al-Shabab".

    Wanasiasa nchini Kenya kwa mara nyingine tena wameitaka Serikali ya Uhuru Kenyatta kuwaondoa haraka wanajeshi wake waliopo nchini Somalia ambapo walikivamia miaka minne iliyopita.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Wanasiasa nchini Kenya kwa mara nyingine tena wameitaka Serikali ya Uhuru Kenyatta kuwaondoa haraka wanajeshi wake waliopo nchini Somalia ambapo walikivamia miaka minne iliyopita.Waziri mkuu wa zamani nchini Kenya Raila Odinga na ambae ni kiongozi wa Baraza la wapinzani amesema akiwa mjini Mombasa kuwa usalama wa Kenya utapitikana endapo wanajeshi wa Kenya waliopo nchini Somalia wataondolewa haraka.
"Serikali ya Kenya ni lazima iwaondoe wanajeshi walioko Somalia na kama hatua hiyo haitachukuliwa mapema basi usalama wa ndani ya Kenya utaendelea kuyumba na Al-Shabab wataendelea na mashambulio yao",alisema Odinga.Ameilaumu umoja wa Afrika kwa kuingiza Kenya vita ambayo ni ngumu na iliyogharimu maisha ya mamia ya raia wa Kenya na kuiyumbisha uchumi wa nchi."Ili kupunguza mashambulio yanayofanyika ndani ya Ardhi yetu ni vyema utawala wa Kenya kuangalia suala hii kwa kuwaondoa wanajeshi wetu walioko Somalia,ni kawaida kwa taifa yeyote kuchukua uamuzi mgumu wa kuokoa maisha ya wananchi wake pamoja na nchi yake kwa ujumla",Odinga.Mashirika mbalimabli ya kiaria pamoja na vyama vya upinzani wanatoa shinikizo kwa Uhuru Kenyatta kuwaondoa Wanajeshi wa Kenya walioko nchini Somalia tangu kufanyika mashambulio ya mji wa Garissa yaliogharimu mamia ya maisha ya wananchi wa Kenya.

Related Items