Maofisa wa Serikali ya FG wauawa katika mji wa Mugadishu na Al-Shabab yadai kuhusika.

Thursday April 09, 2015 - 08:21:45 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2082
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 40
  • 0 1
  • Share via Social Media

    Maofisa wa Serikali ya FG wauawa katika mji wa Mugadishu na Al-Shabab yadai kuhusika.

    Kuna maelezo zaidi yaliopatikana kuhusiana na mauaji ya kupangwa yaliofanyika masaa yaliopita katika Baadhi ya Wilaya zilizopo mikoa ya Banadir na Lower Shabelle nchini Somalia.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kuna maelezo zaidi yaliopatikana kuhusiana na mauaji ya kupangwa yaliofanyika masaa yaliopita katika Baadhi ya Wilaya zilizopo mikoa ya Banadir na Lower Shabelle nchini Somalia.


Watu waliokuwa wamejihami na silaha katika mtaa wa Billaaja Arab Wilayani Shibis wamempiga risasi Mwanama aliyekuwa kiongozi wa mradi ulioitwa ya Ujirani ambao Utawala katika mkoa wa Banadir ulitangaza rasmi miezi kadhaa uliopita mjini Mugadishu.


Duru za kuaminika zinaeleza kuwa Zeynab Ulusow ameuawa ameuawa katika Wilaya ya Shibis,na shambulio lingine iliyofanyika mtaa wa Ali Kamiin Wilayani Wardigley ameuawa Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Eng.Abdullahi aliyekuwa miongoni mwa Maofisa wa Utawala wa Mungaab.Upande mwingine shambulio iliyofanyika Wilaya ya Afgooye imesababisha majeraha mabaya kwa Afisa wa Usalama wa Serikali ya FG wanaojulikana PS ambae alitajwa kwa jina la Abdulahi Muse.


Idhaa ya Kiislaam ya Radio Al Andalus inayomilikiwa na Harakat Al-Shabab Al Mujahideen ilitangaza taarifa ya Mujahidina inayodai kuhusika na mashambulio hayo ya kupangwa yaliofanyika mji wa Mugadishu na Afgooye.
Related Items