Kilonzo Musyoka na Raila Odinga waomba Msaada kwa Marekani ili Wanajeshi wao walioko Somalia waondolewe.

Tuesday April 14, 2015 - 08:05:14 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 3128
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 30
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Kilonzo Musyoka na Raila Odinga waomba Msaada kwa Marekani ili Wanajeshi wao walioko Somalia waondolewe.

    Upinzani nchini Kenya kwa mara nyingine tena wametangaza kuwa Utawala wa nchi hiyo unajiandaa kuwaondoa Wanajeshi wake walioko Somalia ambapo walikaa kwa muda wa miaka minne kwa uvamizi wa kijeshi.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Upinzani nchini Kenya kwa mara nyingine tena wametangaza kuwa Utawala wa nchi hiyo unajiandaa kuwaondoa Wanajeshi wake walioko Somalia ambapo walikaa kwa muda wa miaka minne kwa uvamizi wa kijeshi.


Baada ya kikao kilichofanyika mjini Nairobi ambapo Wabunge kutoka Serikali ya Marekani walishiriki kwenye kikao hicho na kutangazwa kuwa Serikali ya Kenya itawaondoa Wanajeshi wake kutoka Somalia.


Naibu mkuu wa chama cha CORD Kilonzo Musyoka ameliomba Serikali ya Marekani kuisaidia Kenya ili kuweza kuwaondoa Wanajeshi wake kutoka nchini Somalia.Raila Odinga na mwenzake Musyoka wamezungumza na vyombo vya habari baada ya kikao hicho na kuelezea kuwa Serikali ya Kenya haiweza kuhakikisha usalama wa nchi yake ingali Wanajeshi wa KDF wakiwa baado wapo Somalia.


Wabunge wawili kutoka Serikali ya Marekani wamesema Ombi hilo kutoka kwa wanasiasa wa chama cha CORD watawasilisha mbele ya viongozi wa Serikali ya Washington ili kuweza kuisaidia Serikali ya Kenya Gharama ya kuwaondoa Wanajeshi wake kutoka katika Ardhi ya Somalia.


"Ombi hili kutoka kwa  Wanasiasa la kuisaidia Serikali ya Kenya ili iweze kuwarejesha Wanajeshi wake ni hatua inayohitaji mashauriano zaidi",alisema Chris Coons.


Kauli hii ya Chama cha upinzani cha CORD inakinzana na Kauli ya Makamu wa Rais wa Kenya Wiliam Ruto aliyedai kuwa Wanajeshi wa Kenya wataendelea kuwepo Somalia na kuendelea kupambana na Harakat Al-Shabab Al Mujahideen.

Related Items