Mhalifu Haftar aiomba Serikali ya Jordan ili kusaidiwa kupambana na wapiganaji wa Kiislaam nchini Libya.

Wednesday April 15, 2015 - 10:43:31 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2642
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 45
  • 0 1
  • Share via Social Media

    Mhalifu Haftar aiomba Serikali ya Jordan ili kusaidiwa kupambana na wapiganaji wa Kiislaam nchini Libya.

    Kwa mara ya kwanza Mhalifu wa kivita Khalif Haftar anaepigana na waislaam nchini Libya ameanza matembezi ya kimataifa huko akivalia jezi la cheo cha Mkuu wa Jeshi wa Libya.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kwa mara ya kwanza Mhalifu wa kivita Khalif Haftar anaepigana na waislaam nchini Libya ameanza matembezi ya kimataifa huko akivalia jezi la cheo cha Mkuu wa Jeshi wa Libya.Haftar amefika mji Mkuu wa Amman Jordan na kukaribishwa vilivyo na Mfalme wa nchi hiyo Abdallah Bin Husein,Shirika la habari la Urdun limearifu kuwa Haftar ameomba msaada wa kijeshi na Silaha ili aweze kuwashinda kile alichokiita "Magaidi" wa Libya.Serikali ya Jordan iliyo na mahusiano mazuri Marekani na Uingereza imeahidi kulivalia njuga Ombi la Haftar la kupigana na wapiganaji wa Kiislaam wanaopigana Libya ambapo miaka ya hivi karibuni walikuwa wakijisambaza miji mikubwa ya nchi hiyo.


Mataifa ya Magharibi na Serikali za muungano wa nchi za kiarabu wanalaumiwa kulisaidia baadhi ya Maofisa waliokuwa katika Serikali ya Muamar Qadafi ili kuwaondoa wapiganaji Mujahidina wasiokubali Ukoloni katika nchi ya Libya.

Related Items