Serikali ya Tanzania yaendelea na vita vya kiaqida,watoto 115 wakatishwa Masomo ya Qur'an Dodoma.

Saturday April 18, 2015 - 22:44:10 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 3878
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 43
  • 1 2
  • Share via Social Media

    Serikali ya Tanzania yaendelea na vita vya kiaqida,watoto 115 wakatishwa Masomo ya Qur'an Dodoma.

    Serikali kibaraka ya Tanzania baado imeendelea na vita vyake vya kiakili na Aqida dhidi ya Vizazi vijavyo vya Uislaam nchini humo.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Serikali kibaraka ya Tanzania baado imeendelea na vita vyake vya kiakili na Aqida dhidi ya Vizazi vijavyo vya Uislaam nchini humo.Habari kutoka Mkoa wa Dodoma nje kidogo na mji wa Dar Es Salaam zinaeleza kuwa watoto wapatao 115 waliokuwa wakisoma vituo mbalimbali vya kuhifadhisha Qur'an wakitolewa kwa nguvu.Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,David Misime amesema wanafanya uchunguzi katika vituo hivyo kutokana na kuhusika kuendesha vituo hivyo kinyume na Sheria ya nchi.


"Juzi saa sita usiku tulifanya upekuzi katika vituo vitatu,katika kituo cha kwanza tukafanikiwa kuwakuta watoto zaidi ya 63,kati yao 46 ni chini ya miaka 18,na kituo cha pili tukakuta watoto 40,kati yao walio chini ya umri wa 18 walikuwa 12,kituo cha tatu tuliwakuta watoto 7,kati yao walio chini ya umri wa miaka 18 ni 5",alisema Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David Msime.


Katika Msako huo jumla ya watoto wa kiislaam 115 wamesimamishwa Masomo yao kwa kisngizio cha kwenda kusoma elimu ya Sekula,hatua hii imewashangaza maelfu ya waislaam waishio nchini Tanzania huko Mashekhe wakilinyamizia  kimya na kutozungumzia suala hili kwenye Mimbari ya Misikiti mbalimbali yaliodhibitiwa na Serikali.


"Uchunguzi unaendelea na yeyote atakaeguswa na ushaidi atachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa Mahakamani wakiwemo wazazi walioruhusu watoto wao kuwaachia na kuwapeleka katika vituo hivyo",alisema Kamanda Msimo.


Hata hivyo Shekhe mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab kwa upande wa Bakwata amelikemea Msako huo na vitendo vya Polisi na kutaja ni kinyume na taratibu na Sheria ya nchi.


"Hayo ni vituo vya kuwahifadhisha na kuwafundisha watoto wa kiislaam dini yao hasa Qur'an na zilianza tokea zamani na wala hakuna Dhambi na yanafanywa na Ulimwenguni kote,Polisi haina Mamlaka ya kufunga Madarsa za Waislaam",alisema Shekhe Mustaf Rajab.


Hatua hii mpya ya Serikali ya Tanzania iliyoingia mkataba wa kupambana na Uislaam mwaka 2002 na kupitisha Bungeni inatajwa huenda ikazalisha vijana watakao chukizwa na hatua hii mpya na kuanza mapambano ya nguvu na Serikali pamoja na wakristo kama ile ya Nigeria.

Related Items