Afisa wa Serikali ya Kenya atekwa katika mji wa Mandera.

Thursday April 23, 2015 - 22:40:49 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 4494
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 45
  • 2 0
  • Share via Social Media

    Afisa wa Serikali ya Kenya atekwa katika mji wa Mandera.

    Habari iliyotufikia kutoka katika miji ya Kaskazini Mashariki nchini Kenya khususan katikati mwa maeneo ya mji wa Madera na Al Arabia zinaaifu kuwa watu waliokuwa na silaha wamefanya shambulio na kusimamisha Basi waliokuwemo Abiria au wasafiri.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Habari iliyotufikia kutoka katika miji ya Kaskazini Mashariki nchini Kenya khususan katikati mwa maeneo ya mji wa Madera na Al Arabia zinaaifu kuwa watu waliokuwa na silaha wamefanya shambulio na kusimamisha Basi waliokuwemo Abiria au wasafiri.Habari zaidi zinaeleza kuwa watu hao waliofanya shambulio hilo baada ya kusimamisha basi hilo walianza kufanya upekuzi ndani ya Basi na kuanza kuwateremsha Abiria na kisha kuondoka nae Afisa mmoja wa Serikali katika County ya Mandera na baadhi ya vijiji vilio chini ya County hiyo.Watu hao waliotekeleza shambulio hilo inaarifiwa waliondoka na Afisa huyo na kuiruhusu Gari hilo na Abiria wake waliokuwemo kwenye Basi hilo,mpaka sasa haijajulikana walikoenda nae Afisa huyo wa Serikali ya Kenya na hakuna maelezo yeyote kwa kikosi gani kilichotekeleza shambulio hilo.


Vyombo vya habari nchini Kenya vimewanukuu baadhi ya viongozi upande wa usalama wamethibitisha kutokea shambulio hilo iliyomteka kiongozi wa Serikali ya Utawala wa mji wa Mandera iliyo sehemu ya Ardhi inayokaliwa kwa Mabavu.

Related Items