Sh.Kundecha "Tunaipa Serikali siku 15 kuwaachia waislaam wote wanaozuiwa kwa kesi za Ugaidi".

Wednesday April 29, 2015 - 23:50:25 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 5707
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 51
  • 1 0
  • Share via Social Media

    Sh.Kundecha "Tunaipa Serikali siku 15 kuwaachia waislaam wote wanaozuiwa kwa kesi za Ugaidi".

    Hatua ya Serikali kibaraka nchini Tanzaia kuanza mapambano mapya dhidi ya waislaam wanaoishi nchini humo imelaaniwa vikali na viongozi mbalimbali wa waislaam nchini.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Hatua ya Serikali kibaraka nchini Tanzaia kuanza mapambano mapya dhidi ya waislaam wanaoishi nchini humo imelaaniwa vikali na viongozi mbalimbali wa waislaam nchini.Jumuia na Taasisi za Kiislaam nchini Tanzania leo imetoa kauli yake kuhusiana na mbinu mpya ya Serikali Kibaraka yalio dhidi ya Waalimu na vituo vya kuhifadhisha Qur'an pamoja na Watoto Kuachishwa Masomo yao kwa kisingizio kisichakuwa na mashiko.Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya  hiyo Shekhe Mussa Kundecha ambayo ni muunganiko wa Taasisi 11 za dini ya kiislam nchini Sheikh Mussa Kundecha wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema  wamechoka na kuonewa na Jeshi la Polisi kitendo cha kuvamia Misikiti mbali mbali nchini na kuwabambikizia Mashekhe Kesi za Ugaidi.


"Tumempa siku 15,mkuu wa Jeshi la Polisi nchini awe amewaachia mara moja  viongozi wetu waliokamatwa kwa kesi zisizo kuwa na kichwa na miguu,lasivyo akikaidi tutaitisha maandamo makubwa yatakayoitikisa nchi nzima ambayo yatakuwa ni ya kupinga uonevu huu”,alisema Shekhe Kundecha.


Shekh Kundecha ameongeza kuwa  mbali na Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi hao ,Lakini jeshi hilo limeshindwa kuwaachia kwa Dhamana viongozi hao, wakati huo huo amesema Jeshi hilo likiwaachia kwa Dhamana Maaskofu walio na silaha na wanaotoa lugha za kichochezi akiwamo Askofu Josephat Gwajima.

 "Huu ni uonevu gani tunafanyiwa na Serikali hii kwani Sheikh Ponda kwa sasa ni miaka miwili yupo ndani sio kwasababu ya Amri ya Mahakama bali ni ya Amri ya muendesha Mashtaka DPP eti kwa kutoa maneno ya kichochezi lakini kesi hiyo hiyo anayesema ni ya Uchochezi inaendana na Askofu Gwajima pamoja Viongozi wengine wa Dini ya Kikristo ,lakini wako huru vipi Shekhe Ponda”Amehoji Sheikh Kundecha.


Aidha,Sheikh Kundesha huku akiongea kwa Uchungu amesema kwa sasa Jumuiya hiyo imesikitishwa na kitendo cha kuizika Dini ya Kiislam nchini kwa Jeshi la Polisi kuendeleza kuwakamata Walimu wanaofundisha watoto wa Dini hiyo kwenye Madrasa na kuwapa kesi mbali mbali.

"Kule moshi mkoani Kilimanjaro watoto na Walimu wa Madrasa wamekamatwa kama ilivyokuwa Mkoani Mtwara Mwalimu wa  Madrasa  bado wanashikiliwa na Polisi kwa kuwa na watoto wanawafundisha Dini ya Kiislam "


"Dodoma watoto wa tatu wa madrasa,Walimu wao na mwenye Nyumba wanakowafundisha watoto dini ya Kiislam waliwakamata na kupelekwa kituo cha polisi kuhojiwa na kuchukuliwa kama wahalifu wengine hivi nia ya serikali ni ipi”ameendelea kuhoji.


Vilevile Sheikh huyo amewataka waislam kujitokeza mnamo tarehe 15/05/2015 kwenye Maandamano hayo makubwa kwa lengo la kupaza Sauti zao ili Dunia isikia mateso wanayoyapata Waislam wenzao wa Tanzania. 


Serikali Kibaraka ya Tanzania ni sehemu ya Mataifa yanayopambana na Uislaam,huko ikiwashikilia kwa dhulma viongozi kadhaa wa waislaam kwa kisisngizio cha Ugaidi na wengine hata kuawa.

Related Items