Askofu Niwemwugizi:"Waislaam wa Tanzania ni Mawakala wa Ugaidi"

Thursday April 30, 2015 - 00:05:36 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 5000
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 44
  • 2 2
  • Share via Social Media

    Askofu Niwemwugizi:"Waislaam wa Tanzania ni Mawakala wa Ugaidi"

    Matamshi ya Chuki dhidi ya Uislaam na Waislaam yamendelea kushika kasi nchini Tanzania hasa baadhi ya matamshi hayo yakitolewa wazi wazi na viongozi wa Kikristo na Wanasiasa mbalmbali.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Matamshi ya Chuki dhidi ya Uislaam na Waislaam yamendelea kushika kasi nchini Tanzania hasa baadhi ya matamshi hayo yakitolewa wazi wazi na viongozi wa Kikristo na Wanasiasa mbalmbali.


Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Seveline Niwemugizi, amesema baadhi ya Waislaam nchini Tanzania wanafadhili vitendo vya kigaidi vinavyoendelea kutokea duniani.Askofu Niwemugizi alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifadhili vitendo vya ugaidi na vita takatifu,(Jihaad) ama kwa kujua au kutojua!


Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na baadhi ya wakristo wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera katika mafunzo walioyaita kuwa ni maalumu ya elimu ya uraia kwa wakristo kuhusu mapungufu yaliyomo kwenye katiba inayo pendekezwa kabla ya kuipigia kura.


"Napenda kuwatahadharisha sana Watanzania...wengi wetu wamekuwa wakifadhili ugaidi na vita takatifu, lakini baadhi yao hufadhili kwa kutojua na wengine kufahamu wanachokifanya kwa sababu ni mkakati wa muda mrefu ulioandaliwa kwa lengo maalumu,” alisema Askofu Niwemugizi.


"Ninasema haya siyo kwa bahati mbaya, umefanyika uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha undani wa maneno haya...kama mimi kuna kitu ninakielewa na nikakaa nacho kimya pasipo kuwataarifu nitakuwa ninafanya dhambi mbele ya Mungu wetu aliyeniagiza kuwachunga kondoo wake,” alisema.


Wakristo na wanasiasa nchini Tanzania wamekuwa na nyimbo ya muda mrefu wa kuomba Ugaidi ambalo maana yake halisi ni Uislaam uliobeba Dini kamili,kazi iko kwa waislaam nchini na namna wanaovyoichukulia kauli hizi na mkakati wa Serikali wa kuvamia Madrasa za kiislaam na kuwaachisha Masomo vijana wa Kiislaam.

Related Items