Wanajeshi wa Kenya wafanya mauaji dhidi ya Waislaam katika mji wa Wajeer na Kaburi la pamoja lagundulika.

Sunday May 03, 2015 - 23:50:29 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 6036
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 45
  • 1 0
  • Share via Social Media

    Wanajeshi wa Kenya wafanya mauaji dhidi ya Waislaam katika mji wa Wajeer na Kaburi la pamoja lagundulika.

    Habari kutoka Mkoa wa Kaskazini Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na Utawala wa Kenya zinaarifu kuwa Kaburi la watu waliozikwa pamoja limegundulika nje ya mji wa Wajeer.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Habari kutoka Mkoa wa Kaskazini Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na Utawala wa Kenya zinaarifu kuwa Kaburi la watu waliozikwa pamoja limegundulika nje ya mji wa Wajeer.Wakaazi wamesema wamegunduwa Shimo kubwa waliozikwa watu 11 kwa siri ambao walikuwa ni waislaam wanaotoka katika Mji huo wa Wajeer.Habari zaidi zinaeleza kuwa watu waliopatikana maiti zao ni pamoja na Mashekhe ambao katika miezi yaliopita walikuwa wametoweka na inaaminika wameuawa na Wanajeshi wa Kenya hasa kitengo chake cha kupambana na kile wanachokiita Ugaidi. 


Kaburi hilo la pamoja limegundulika katika kijiji kilicho katikati mwa miji ya Wajeer na Mandera,Makumi ya familia na jamaa ya watu waliouawa wamefika eneo hilo na wamesema wataandamana mbele ya vituo vya Serikali ya mji wa Wajeer.


Duru zinaeleza kuwa idadi ya watu 17 wengine hawajulikani waliko na inaaminika nao pia wameuawa na Maaskari hao wa kupambana na Uislaam nchini Kenya.


Serikali ya Kenya imekuwa maarufu kwa Mauaji ya Waislaam khususan jamii ya Kisomali waishio kwenye mikoa ya kaskazini Mashariki na itakumbukwa Mauaji ya kihistoria ya Wagala na Garissa miaka 30 yaliopita ambapo Maelfu ya Wasomali waliuawa. 

Related Items