Utawala wa Somaliland yampiga Marufuku Sheikh Adan Sunne kutoa Da'awah katika Misikiti yalioko mji wa Hargeysa.

Thursday May 07, 2015 - 22:31:03 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 5900
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 50
  • 4 2
  • Share via Social Media

    Utawala wa Somaliland yampiga Marufuku Sheikh Adan Sunne kutoa Da'awah katika Misikiti yalioko mji wa Hargeysa.

    Utawala uliojiita Somaliland umetangaza rasmi kumpiga marufuku kutoa Da'awah au Darsa inayowaeleimisha Umma wa Kiislaam katika mji wa Hargeysa Sheikh Adan Sune ambae ni miongoni mwa Mashekhe wanaodhihirisha Da'awah ya haqi.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Utawala uliojiita Somaliland umetangaza rasmi kumpiga marufuku kutoa Da'awah au Darsa inayowaeleimisha Umma wa Kiislaam katika mji wa Hargeysa Sheikh Adan Sune ambae ni miongoni mwa Mashekhe wanaodhihirisha Da'awah ya haqi.


Waziri anae husika Masuala ya Dini katika utawala wa Somaliland amesema Shekhe hutoa Da'awah na Darsa za kidini iliyowafanya waislaam wengi kupenda Mawaidha yake na kisha kuanza kuwachukia wageni wanaokuja kwa lengo la kufanya Utalii mji wa Hargeysa.Utawala huo unaoupiga vita Uislaam wa "Somaliland" umetoa Amri kwa bodi ya Shirika la Al Hudaa inaojihusisha na masuala ya Kida'awah kumzuia Sheikh Adan Sune kutoa Darsa yeyote ya Kidini au kutoa Qutba siku za Ijumaa katika Misikiti yote iliyo chini ya Bodi hiyo.


"Kwa yeyote anaehusika natoa Amri ya kumzuia kutoa Darsa au Mawaidha yeyote ya Kidini katika misikiti yalio chini yenu kwa Sheikh Adan Abdi Warsame mpaka hapo mtakapo pata Amri nyingine,hata hivyo ni lazima kutujulisha Mashekhe wengine watakaoingia kutoa Mawaidha kama sisi tukiwa kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Dini",alisema Khalil Abdulahi ambae ni Waziri wa Masuala ya Dini katika utawala wa Somalilanda.


Sheikh Adan Sune ni miongoni mwa Mashekhe wasiogopa kudhihirisha Da'awah ya haqi na kuwausia jamii ya Mji wa Hargeysa kuzuia Munkari na kuamrisha Mema,Mawaidha na Qutba anayotoa Shekhe imewachukiza sana Mawaziri na Maofisa wa Utawala Fisadi wa Somaliland na kusababisha Shekhe kufungwa mara kadhaa.


Ni mara ya kwanza kwa Sheikh Adan Sune kupigwa Marufu katika kazi zake za ulinganizi wa Da'awah katika Jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Ardhi ya Somalia,mwezi uliopita wanajeshi wa RRU walimtoa Shekhe kutoka nyumbani kwake kwa nguvu na baada ya masiku kadhaa alipata kuachiliwa.Liban Abdi Jehow

SomaliMemo,Mugadishu

Related Items