UFAFANUZI:Shambulio uliosababisha hasara yafanyika katika Makao Makuu ya mji wa Banadir.

Friday July 04, 2014 - 16:17:51 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 1552
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 0 0
  • Share via Social Media

    UFAFANUZI:Shambulio uliosababisha hasara yafanyika katika Makao Makuu ya mji wa Banadir.

    Watu waliokuwa wamejihami na Silaha nzito ambapo wanaodhaniwa kuwa ni Vikosi vya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen walipambana na Wanamgambo wa Serikali ya FG jana usiku.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Moshi ukiwa umetanda angani katika mji wa Mugadishu.
Watu waliokuwa wamejihami na Silaha nzito ambapo wanaodhaniwa kuwa ni Vikosi vya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen walipambana na Wanamgambo wa Serikali ya FG jana usiku.

Mapema jana usiku kulifanyika mashambulio yaliodumu takriban dakika 35 kwenye Makao makuu mpya wa Utawala wa Halmashauri ya Mkoa wa Mugaishu au Banadir uliopo kwenye Barabara zinazoungana katia ya Yaqshiid na Huriwaa mjini Mugadishu.


Mashuhuda wanasema washambuliaji walikuwa na Silaha za kuweka Begani ambapo walizitwanga kwenye Majengo hayo ya Makao makuu ya Mji wa Mugadishu na baada ya muda mfupi ukafuatia Makabiliano ya ana kwa ana kati ya Washambuliaji na Maaskari wa Serikali ya FG.

Vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa Askari mmoja aliykuwa akilinda kwenye majengo hayo ni miongoni mwa watu waliouawa na washambuliaji na Maaskari wengine 5 wamejeruhiwa vibaya kufuatia makabiliano hayo ya jana usiku.


Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa kwenye majengo ya Makao makuu,hali ya utulivu umerejea katika Wilaya ya Yaqshiid na Huriwaa ambapo makabilian yalifanyika jana usiku.


Aidha ofisi ya Usalama wa Taifa wanaojulikana PS yalioko eneo la Warshada Barafunka mjini Mugadishu imeshambuiwa,pia Maaskari Polisi waliokuwa wakilinda Makao ya Wilaya ya Dayniile nao wamekutana na Mashambulio kutoka kwa watu waliokuwa wamejihami na Silaha.

Viongozi wa Harakat Al-Shabab Al Mujahideen walitishia kuzidisha Mashambulio mjini Mugadishu ndani ya Mwezu mtukufu wa Ramadhan na vitisho hivyo inaonekana kuwa yamekuwa kweli.Liban Jehow AbdiSomaliMemo,MugadishuRelated Items