Uharbifu uliofanywa kwenye Maktaba ya Darul Arqam na Vifaa pamoja na Pesa kuibiwa na Maaskari waliomvamia Sheikh Abuu Ismail (Maelezo).

Monday July 14, 2014 - 23:51:45 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 5041
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 4 0
  • Share via Social Media

    Uharbifu uliofanywa kwenye Maktaba ya Darul Arqam na Vifaa pamoja na Pesa kuibiwa na Maaskari waliomvamia Sheikh Abuu Ismail (Maelezo).

    Kuna maelezo zaidi yaliopatikana kuhusiana uvamizi uliofanywa na Maaskari wa kupambana na Uislaam kwenye nyumba na Maktaba ya Sheikh Abuu Ismail Ibrahim mkoani Mwanza nchini Tanzania.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kuna maelezo zaidi yaliopatikana kuhusiana uvamizi uliofanywa na Maaskari wa kupambana na Uislaam kwenye nyumba na Maktaba ya Sheikh Abuu Ismail Ibrahim mkoani Mwanza nchini Tanzania.Tovuti ya Kislaam ya SomaliMemo imefanya juhudi ya kuwasiliana na Ndugu pamoja na Wanafunzi wa Shekhe na kudokezewa jinsi Maaskari hao walivyokiuka haki za Binadaamu dhidi ya Waislaam mkoani Mwanza.

Habari kutoka Jijini Mwanza zinaeleza kuwa Shekhe hadi kufikia leo siku ya J/tatu hakujulikana alikopelekwa,na mmoja wa maofisa wa Polisi waliohusika kumvamia Sheikh Abuu Ismail usiku wa kuamkia Jumapili alisema na kuomba kutotajwa jina lake kuwa Shekhe hayuko Mwanza na Maaskari walihofia kumweka Mwanza kutokana na khofu ya Waislaam.
"Ndugu yangu nakuambia Ustazi hayupo Mwanza huenda amepelekwa kwingine kwasababu ya Usalama wake si unajua Waislaam wakiamua waweza kufanya lolote kwa Maaskari!",alisema afisa huyo wa Polisi.

Pia Askari huyo alizidi kuidokezea Mmoja wa Maikhwa waliokwenda kufutilia Sheikh Abuu Ismail anakoshikiliwa kuwa"Unajua Ustaz alitakiwa kukamatwa tokea siku ya Ijumaa katika Msikiti wa Luqmaan laikini tulihofia Waislaam walikuwa wamemzunguka kwa wingi,na katika kumfutilia siku ya pili tulikwenda hadi kwenye Msikiti wa Mhandu Igoma lakini pia hatukumpata".
Maaskari hao Madhalimu walifanya uharibifu mkubwa katika Maktaba ya Shekhe kwa kuvunja mlango wa kioo wa kuingilia kwenye Maktaba huo na kisha kuingia hadi ndani ya Maktaba wakianza kupekua na kutupa tupa vitabu vya Dini.

Taarifa rasmi ilioipata SomalMemo kuhusiana na uvamizi huo wa Madhalimu dhidi ya Shekhe inaeleza kuwa Maaskari 6 walikuwa ni kutoka nje ya Mkoa wa Mwanza ambapo wengine waliokuwa zaidi ya 4 walikuwa ni wenyeji wa mji wa Mwanza,usiku huo baada ya kumpiga vibaya mwanafunzi wa Shekhe waliondoka nae pamoja na Shekhe mwenyewe na Laptop,Printer,na Pesa alizokuwa akizitunza kwenye Maktaba.

Hata hivyo Maaskari hao hawakuacha Gari ndogo aina ya Suzuki Escudo aliyokuwa akitumia katika kazi yake Da'awah na kwenda kuegesha ndani ya kituo kikuu cha Polisi Jijini Mwanza.

Katika siku za hivi karibuni vyombo vya Habari vinavyotumiwa na Maadui wa Uislaam ambazo zingine zikijinasibisha na Uislaam walikuwa wakihoji juu ya kutokamatwa kwake shekhe Abuu Ismail,na baada ya kukamatwa Shekhe wamekaa kimya na kuficha uovu wa Maaskari wa Serikali kibaraka wa Tanzania kwa kumvamia usiku wa manane. 

Serikali ya tanzania imejihusisha mmoja kwa mmoja katika kuidhulumu na kuwadhulumu waislaam na kujiunga na mataifa yanayoipiga vita Uislaam ikiwa ni pamoja na kuwua Mashekhe na kuwatia kizuizini bila hatia yeyote na itakumbukwa Shekhe Maarufu Issa Ponda na wengine wengi wanateseka ndani ya Magareza yaliopo nchini.
Abdallah Al Bajuni


SomaliMemo,Dar Es Salaam


Related Items