PICHA:Maofisa wengine wauawa kwenye mlipuko na kwa kupigwa Risasi katika mji wa Mugadishu.

Friday July 18, 2014 - 01:41:57 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 1938
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 0 0
  • Share via Social Media

    PICHA:Maofisa wengine wauawa kwenye mlipuko na kwa kupigwa Risasi katika mji wa Mugadishu.

    Kumepatika maelezo zaidi kuhusiana na mauaji ya kupangwa na mlipuko uliofanyika jana katika baadhi ya maeneo mbalimbali mjini Mugadishu.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kumepatika maelezo zaidi kuhusiana na mauaji ya kupangwa na mlipuko uliofanyika jana katika baadhi ya maeneo mbalimbali mjini Mugadishu.
Watu waliojihami na Silaha walimwua kwa kumtwanga Risasi Afisa aliyekuwa na cheo cha juu katika jeshi la Polisi la Serikali ya FG Col.Afgaduud mda mchache baada ya mauaji yaliofanyika Wilaya ya Wadhajir ulisikika mlipuko mkubwa kusini mwa mji wa Mugadishu.
Gari Ndogo aina ya Carib iliyokuwa ikitembea eneo la Uwanja wa Tarabuunka ililengwa na mlipuko upande wa mbele wa Gari hilo,walioshuhudia wanasema watu wote waliokuwemo kwenye Gari hili wameuawa na wengine kujeruhiwa vibaya.

Embedded image permalink
Kwenye shambulio hilo la Bomu aliuawa Afisa mmoja wa Jeshi la Polisi la Serikali ya FG ambayo alitajwa kwa jina la Abdullahi Siyad.

Upande mwingine jana jioni katika Wilaya ya Yaqshiid ameuawa Afisa aliyekuwa kwenye Ofisi ya Utawala wa Mkoa wa Banadir aliyetajwa kwa jina la Mahamed Abtidoon.
Mauaji ya kupangwa na milipuko yanayoilenga Maofisa wa Serikali na Wanajeshi wa Kigeni yaliojiita AMISOM yamezidi kuongezeka ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhaani.

Liban Jehow Abdi


SomaliMemo,Mugadishu


Related Items