PICHA:Watu walio na silaha washambulia kituo cha Polisi na kuchukua Silaha katika mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

Thursday June 12, 2014 - 11:14:56 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 7467
  • (Rating 3.0/5 Stars) Total Votes: 1
  • 2 0
  • Share via Social Media

    PICHA:Watu walio na silaha washambulia kituo cha Polisi na kuchukua Silaha katika mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

    Habari kutoka mkoa wa Pwani nchini Tanzania zinaeleza kuwa watu waliokuwa wamejihami na silaha za Jadi wamevamia kituo kidogo cha Polisi na kufanya mauaji ya Askari mmoja na kuchukua Bunduki tatu za SMG na risasi zake.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Habari kutoka mkoa wa Pwani nchini Tanzania zinaeleza kuwa watu waliokuwa wamejihami na silaha za Jadi wamevamia kituo kidogo cha Polisi na kufanya mauaji ya Askari mmoja na kuchukua Bunduki tatu za SMG na risasi zake.
Tukio hili lilifanyika mapema leo asubuhi kwenye kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani,watu waliokuwa wamejihami na Silaha za Jadi walifanya shambulio kwenye kituo cha Polisi cha kimanzichana.

Washambuliaji walimwua kwa kumshambulia kwa mapanga Askari aliyetajwa kwa jina la Joseph Ngonyani na kisha kuchukua Bunduki lake aina ya SMG pamoja na Bunduki la Askari mwingine waliomjeruhi na ndipo walipoanza kutumia Bunduki kwa kuwashambulia Maaskari wengine waliokuwepo eneo la Kituo cha Polis.

somalimemo

Maaskari waliojeruhiwa ni wawili ambapo walikimbizwa Hospitali ya muhimbili kwajili ya matibabu zaidi,jumla ya Bunduki zilizochukuliwa na washambuliaji ni 3 aina za SMG pamoja na Risasi zaidi ya 50.

Maofisa wa Polisi wamethibitisha kutokea tukio hilo na kusema kuwa wameanza msako kwanzia maeneo ya Kituo cha Polisi,Mkuranga,Rufiji,Kibaha na Dar Es Salaam.

Related Items