UFAFANUZI:Mlipuko uliowathiri Wanajeshi wa Djibuti yafanyika mji wa Buula Barde.

Thursday June 12, 2014 - 22:14:56 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 1794
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 0 0
  • Share via Social Media

    UFAFANUZI:Mlipuko uliowathiri Wanajeshi wa Djibuti yafanyika mji wa Buula Barde.

    Kumepatika maelezo zaidi kuhusiana mlipuko mkubwa ulioitikisa mji wa Buula Barde iliyo mkoa wa Hiraan katikati mwa Ardhi ya Somalia.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kumepatika maelezo zaidi kuhusiana mlipuko mkubwa ulioitikisa mji wa Buula Barde iliyo mkoa wa Hiraan katikati mwa Ardhi ya Somalia.
Habari kutoka mji wa Buula Barde zinaeleza kuwa kumelengwa mlipuko kwenye Gari waliokuwemo Maaskari wa Djibuti,Gari hilo ilikuwa ndani ya Uwanja wa Ndege wa mji huo ambapo ndio Uwanja pekee unaotumiwa na Wanajeshi wa Djibuti kwa kuingizia shehena zao za silaha na vifaa vingine vya kijeshi.

Wakaazi wa mji huo wamesikia kishindo cha mlipuko mkubwa na baada ya muda mchache mawasiliano ulikatika lakini leo nyakati ya Adhuhuri mawsiliano ulirejea kama kawaida baada ya Wanajeshi wa Djibuti kuchukua miili ya Wanajeshi wao na majeruhi kadhaa kwenda upande wa Baladweyne.


Duru ziliarifu kuwa Wanajeshi 3 wa Djibuti waliauawa na Mlipuko huo na wengine 4 wakijeruhiwa vibaya,mlipuko huo uliolengwa ulikuwa bomu la kutegwa Ardhini kama walivyonukuliwa Maofisa wa Polisi wa Serikali ya TFG.

Mji wa Buula Barde ilitoka mikono ya Wilayatul Islamiah ya Hiraan mwezi Machi mwaka huu na mji huo ulichukuliwa na Wanamgambo wavamizi kutoka Djibuti.

Liban Jehow Abdi
SomaliMemo,Mugadishu
 

Related Items