Sumaya ni mwanadada wa Kislaam mwenye mtoto wa umri wa miezi 10 anaedhulumiwa na Serikali ya Tanzania.

Friday August 08, 2014 - 20:47:54 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 4290
  • (Rating 2.0/5 Stars) Total Votes: 2
  • 0 0
  • Share via Social Media

    Sumaya ni mwanadada wa Kislaam mwenye mtoto wa umri wa miezi 10 anaedhulumiwa na Serikali ya Tanzania.

    Gazeti mmoja la kila siku linalotoka nchini Tanzania limeandika kwa majonzi makubwa huko ikipa kichwa cha habari kuwa "Vilio na Simanzi yasikika eneo la Mahakama" ambao ilihusiana na mwanadada Sumaya aliyetuhumiwa kukutwa na silaha pamoja n

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Gazeti mmoja la kila siku linalotoka nchini Tanzania limeandika kwa majonzi makubwa huko ikipa kichwa cha habari kuwa "Vilio na Simanzi yasikika eneo la Mahakama" ambao ilihusiana na mwanadada Sumaya aliyetuhumiwa kukutwa na silaha pamoja na mabomu kama walivyodai Maofisa wa Kupambana na Uislaam mkoani Arusha.
Sumaya ambae ni mke wa Yusuf Ally ambae kwa pamoja walikamatwa na mtoto wao mwenye umri wa miezi 10 na kuwekwa kizuizini kwa tuhuma za kukutwa na mabomu na Silaha nyumbano kwao Arusha.
Gazeti hilo liliendelea kusema kuwa "sauti za vilio zilisikika na nyuso za simanzi zilionekana baada ya mtuhumiwa Sumaya ambae ni mke wa Yusuf Ally wanaotuhumiwa kwa kukutwa na mabomu nyumbani kwao kushuka ktk gari dogo aina ya Vits yenye namba za usajili T727 CVL akiwa na mwanawe wa miezi 10.
Vilio hivyo vilitokana na umri mdogo wa mtoto huyo huko mama yake akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari kanzu wa kike ambapo walimpeleka hadi chumba cha mahabusu cha Mahakama hiyo na kumfungia yeye na mwanae,hata hivyo.
Saa chache baadae simanzi na vilio zaidi vilisikika baada ya mtoto huyo kulia kwa muda mrefu hali iliyosababisha Askari kanzu hao wa kike kuingiwa na huruma na kumwombea Askari wa Magereza kumfungulia mama huyo na mwanae ili aweze kukaa ktk chumba cha Mahakama ambapo Askari hao wa Magereza waligoma kwa Ukaidi mkubwa.
Baada ya Askari Magereza hao kugoma mmoja wa Askari kanzu wa Kike aliwaomba Askari hao wa Magereza kumtoa mtoto mtoto huyo ili ambembeleze wakati akisubiri kesi ambapo ombi hilo lilikubaliwa na mtoto huyo kutolewa na kuendelea kubembelezwa hadi kesi ilipoanza kusikilizwa na kumalizika tarehe 01,August,2014",ilimalizia gazeti hilo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Abuu Ismail kuachiwa


Habari kutoka Jijini Mwanza zinaeleza kuwa baadhi ya Wanafunzi wa Sheikh Abuu Ismail waliodhulumiwa na Maaskari wa kupambana na Uislaam wameachiwa na hivi sasa wako Mkoani Mwanza ambapo walirudishwa wakiwa chini ya ulinzi Mkali kwa usafiri wa Basi kutoka Arusha.Mmoja wa Muislaam aliyesafiri kutoka Arusha alisema niliwaona Vijana waliokuwa na Vilemba na kanzu wakiwa hawana Viatu na baada ya kumwuliza mmoja wao alimweleza kuwa walipata Qadari na wamekamtwa kutokana na tuhuma."Niliwaona vijana wa Kislaam waliovalia Vilemba na walionekana wakiwa hawana wasiwasi kabisa,tuliokutana Singida wakiwa peku huko wakienda msalani nilishikwa na huruma nikatoa Sandoz yangu niliokuwa nayo kwenye Begi nikawapa kwasababu ni waislaam ndugu zangu",alisema Muislaam huyo ambapo kwa jina tumemhifadhi.Da'awah Ndani ya Gereza na Mustafa Kihago na Abuu Ismail uso kwa uso!


Mmoja wa Maikhwa waliobahatika kukutana na Abuu Aisha mmoja wa Wanafunzi waliopata Uhuru wake alieleza kuwa hali ya Sheikh Abuu Ismail na baadhi ya Maikhwa wengine inaendelea vyema na Abuu Ismail ameshaanza kutoa Da'awa akiwa Gerezani huko akiwahimiza waislaam kuwa na subra na kumwomba Allah awaondolee Madhila wanayokutana nayo.Maadui wa Allah huangalia na kupambana na Uislaam bila kuangalia Fikra yako hata kama huna fikra na ulikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakipiga vita Da'awah ya haki basi huenda ikakuta kama iliyomkuta Sheikh Mustafa Kihago baada ya kukamatwa na Maaskari wa kupambana na Uislaam.Mustafa Kihago baada ya kuulizwa tuhuma azlizozitoa kwenye Gazeti mmoja la hapa nchini alidai kuwa yeye hakuwapa taarifa na waandishi walizusha wenyewe ili kuweka fitna baina ya waislaam na yeye kuonekana kuwa mpinzani.
Abdallah Al BajuniĀ 


SomaliMemo,Dar Es Salaam


Related Items