Sheikh Farid "Watu wameumizwa vibaya wanajisaidia haja ndogo damu wiki mmoja hadi mbili iko siku Mahakamani watu wataletwa wakiwa Maiti!".

Friday August 22, 2014 - 23:38:43 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 6993
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 2 0
  • Share via Social Media

    Sheikh Farid "Watu wameumizwa vibaya wanajisaidia haja ndogo damu wiki mmoja hadi mbili iko siku Mahakamani watu wataletwa wakiwa Maiti!".

    Madhila makubwa yamendelea kutendwa na Maaskari wa kupambana na Uislaam dhidi ya Viongozi wa Kislaam waliotekwa kutoka Zanzibaar ambao ni Kisiwa kinachokaliwa kwa Mabavu na Utawala wa Kinasara wa Tanganyika.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Madhila makubwa yamendelea kutendwa na Maaskari wa kupambana na Uislaam dhidi ya Viongozi wa Kislaam waliotekwa kutoka Zanzibaar ambao ni Kisiwa kinachokaliwa kwa Mabavu na Utawala wa Kinasara wa Tanganyika.


Baadhi ya Vyombo vya habari nchini Tanzania zimeandika taarifa za kusikitisha na kuhuzunisha ambapo viongozi muhimu wa Kislaam khususan mfasiri maarufu wa Qur'an Afrika Mashariki Sheikh Mselem Ali wametendewa Vitendo vya Kinyama.Soma hapa chini taarifa ya kusikitisha waliofanyiwa kwa Waislaam.

Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), ametoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi akidai kuwa limewafanyia ukatili kwa kuwapiga, hali inayowafanya baadhi yao wajisaidie damu.


Sheikh Farid alitoa madai hayo jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi ya tuhuma za ugaidi inayowakabili ilipokuwa ikitajwa.


Wakili wa Serikali Mwandamizi, Peter Njike, alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika na wanaomba hati ya kuwachukua washtakiwa saba, akiwamo Sheikh Farid kwa ajili ya mahojiano.


Hakimu Riwa alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Hali hiyo ilisababisha washtakiwa kuomba kutoa maelezo yao.


"Mheshimiwa wametuomba kwenda kutuhoji tena, mara ya kwanza tulipohojiwa, polisi hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu, ni ushenzi na ukatili, walituhoji uchi wa mnyama na kutupiga.


"Kiongozi Mkuu wa Uamsho, Sheikh Mselem Ally Mselem, mwenye heshima, mfasiri wa Kur’ani, alinihadithia alipohojiwa walimfanya nini, tumepigwa na hatukutibiwa, magereza wamejitahidi, lakini hawana nyenzo za matibabu.


"Watu wameumizwa vibaya, mengine hayasemeki, wanajisaidia haja ndogo damu wiki moja hadi mbili, tunaomba tufanyiwe uchunguzi wa afya zetu, ipo siku mahakamani italetwa maiti.


"Tumekamatwa sababu hatutaki Muungano, hiyo ndiyo kesi ya msingi, tunawaambia ukweli katika mihadhara na watu wanatuamini, tunaomba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iletwe mahakamani tuijadili,” alidai Sheikh Farid.


Mshtakiwa wa 12, Salum Alli Salum, aliomba mahakama imwite daktari ili aweze kufanyiwa uchunguzi wa afya yake kwani ameingiliwa kijinai kwa nguvu.


"Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia kinyume cha maumbile, wanaingiza majiti, chupa, wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe.


"Askari ameniingilia kisha akaniingiza jiti mpaka likakatika, kungekuwa na sehemu ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria, waliofanya madhila haya wanawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya,” alidai mshtakiwa huyo.


Baada ya washtakiwa hao kutoa malalamiko yao, mahakama iliwaahidi washtakiwa hao waende wakahojiwe na muda wote watakuwa katika mazingira salama.


Chanzo:Mtanzania

Related Items