VIDEO:Jabhat Al Nusrah yawaachia wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Sunday September 14, 2014 - 12:26:47 in WARBIXINNO/QORALLO XUL AH by Super Admin
  • Visits: 2521
  • (Rating 0.0/5 Stars) Total Votes: 0
  • 0 1
  • Share via Social Media

    VIDEO:Jabhat Al Nusrah yawaachia wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

    Taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha kuwa makumi ya Wanajeshi wa U.N kutoka Fiji waliachiwa huru baada ya kushikiliwa nchini Syria kwa muda mrefu.

    Share on Twitter Share on facebook Share on Digg Share on Stumbleupon Share on Delicious Share on Google Plus

Kikosi cha Wanajeshi wa U.N kutoka Fiji.
Taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha kuwa makumi ya Wanajeshi wa U.N kutoka Fiji waliachiwa huru baada ya kushikiliwa nchini Syria kwa muda mrefu.


Wanajeshi hao wanaofikia 45 walikamatwa kwenye mapigano makali yaliofanyika upande wa mpaka kati ya Syria na Milima ya Al-Jowlani inayoshikiliwa na Mayahudi.Sami Al Ureymi ambae ni miongoni mwa Viongozi wa Jabhat Al Nusra amesema wamewaachia Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ambapo ameongeza kuwa kuwaachia kwa Wanajeshi hao hawakuweka masharti yeyote ingawa walikwisha ahidi kuwaachia hapo awali. Hapo awali Jabhat Al Nusra ilitoa ombi kwa U.N ili kuondolewa kundi lao kwenye Orodha ya Makundi ya Kigaidi lakini ombi hilo halikutekelezwa.Msemaji aliyezungumza kwa Niaba ya Umoja wa Mataifa amethibitisha kuachiwa Wanajeshi 45 wazaliwa wa Fiji na tayari wamekwisha pelekwa Makazi ya 80 la Al Jowlaani.Vyanzo iliyoinukuu televisheni ya kiarabu ya Al Jazeera imesema kuwa kuachiwa kwa Wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa waliokuwa mikononi mwa Jabhat Al Nusra ilikuja baada ya mazungumzo yalioendeshwa mmoja wa mataifa ya Kiarabu ambayo ilikataa kutumiwa jina lake.Umoja wa Mataifa ni eneo linaloandaliwa Vita dhidi ya Waislaam na Uislaam na ni Umoja unaotumiwa kwa Maslahi ya Mataifa ya Magharibi na Amerika.Wanajeshi wa U.N waliopo Milima ya Al Jowlani wamepewa inaifanya Utawala haramu wa Israel kuendelea kuitawala kwa mabavu Ardhi ya Waislaam wa Falasdin.

TIZAMA VIDEO HAPA CHINI


Related Items